Swalah ya kupatwa kwa jua imeswaliwa kimakosa – irudiliwe?

Swali: Kuna mtu aliwaswalisha watu swalah ya kupatwa nje ya mji katika bari ilihali hajui namna yake ambapo akawaswalisha Rak´ah mbili. Walipomaliza swalah wakamjuza wale waliokuwa pamoja naye kwamba swalah yake ni ya kimakosa. Je, airudi swalah yake?

Jibu: Airudi swalah maadamu kupatwa kwa jua bado kunaendelea. Lakini kukisha hakuna haja. Tumeyataja haya katika yale maneno ya kwanza ya kwamba kupatwa kwa jua kukiisha kabla ya watu kuswali, basi swalah isiswaliwe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1123
  • Imechapishwa: 27/04/2019