Swalah ya ´iyd inaswaliwa viwanjani na si misikitini

Swalah ya ´iyd inatakiwa kuswaliwa kwenye jangwa karibu na mji. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali swalah ya ´iyd katika uwanja wa kuswalia ulio karibu na mlango wa al-Madiynah. Abu Sa´iyd amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitoa katika [swalah ya] al-Fitwr na [swalah ya] al-Adhwhaa katika uwanja wa kuswalia.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Haikupokelewa kwamba aliiswali msikiti isipokuwa ilikuwa ni kutokana na udhuru.

Jengine ni kwa sababu kutoka kwenda katika jangwa kunaonyesha zaidi haiba ya waislamu na Uislamu na pia kuonesha zaidi nembo ya dini. Hakuna ugumu katika kufanya hivo kwa sababu ni ´iyd ni kitu kisichokariri kama ilivyo swalah ya ijumaa. Isipokuwa tu msikiti wa Makkah wao wanatakiwa kuswali katika msikiti Mtakatifu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mulakhaswsw-ul-Fiqh (01/268-269)
  • Imechapishwa: 30/07/2020