Sunnah kuswali Rak´ah nne kabla ya ´Aswr

Swali: Ni upi usahihi wa Hadiyth:

“Allaah amrehemu mtu mwenye kuswali Rak´ah nne kabla ya ´Aswr?”

Jibu: Kinachojulikana ni kwamba imetibiti na kwamba haina neno. Kujengea juu ya haya imesuniwa kwa muislamu kuswali Rak´ah nne kabla ya ´Aswr ambapo atatoa salamu kila baada ya Rak´ah mbili. Lakini sio katika Sunnah za Raatibah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (13) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
  • Imechapishwa: 15/02/2020