Mwache mwanamke uliyemuoa Mut´ah!

Swali: Ni ipi hukumu ya ndoa ya Mut´ah na ni ip hukumu ya kutaliki ndani yake?

Jibu: Ndoa ya Mut´ah haijuzu ni batili. Ni kule mtu kuoa kwa muda maalum. Wanakubaliana kwa mfano kuoana mwaka mmoja kisha wakaachana, mwezi mmoja au miezi miwili.

Ndoa hii iliruhusiwa mwanzoni mwa Uislamu kisha baadaye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaikataza na kuifuta na akasema:

“Hakika Allaah ameiharamisha mpaka siku ya Qiyaamah.”

Kama mtu ameoa Mut´ah amwache mwanamke huyo. Kwa sababu ni jambo lina tofauti kwa wanachuoni. Mtu akioa Mut´ah basi ataliki talaka moja kwa ajili ya kutatua tatizo na kuondosha ndoa hii yenye kutatiza. Atoe talaka moja peke yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3548/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B2%D9%88%D8%A7%D8%AC-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%AA%D8%B9%D8%A9-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%B7%D9%84%D8%A7%D9%82-%D9%81%D9%8A%D9%87
  • Imechapishwa: 15/02/2020