Ahmad bin Kaamil amesema:

“Ya´quub bin Shaybah alikuwa akichukua msimamo wa kunyamaza juu uumbwaji wa Qur-aan.”

Alichukua msimamo wa kunyamaza kutoka kwa mwalimu wake Ahmad bin al-Mu´adhdhal. Pia ´Aliy bin al-Ja´d, Musw´ab az-Zubayriy, Ishaaq bin Abiy Israaiyl na jopo la wanachuoni wengine walikuwa wakichukua msimamo wa kunyamaza. Hata hivyo hakukuwa maelfu ya maimamu waliowakhalifu bali maimamu wengine wote wa Salaf na waliokuja baadaye walikuwa ni wenye kukubaliana juu ya kwamba Qur-aan haikuumbwa na kwamba Jahmiyyah ni makafiri. Tunamuomba Allaah usalama katika dini yetu.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/478)
  • Imechapishwa: 22/11/2020