Bora ni kusoma Qur-aan msikitini kwa sauti au kimyakimya?

Swali: Bora ni kusoma Qur-aan msikitini kwa sauti au kimyakimya?

Jibu: Bora msikitini ni kusoma Qur-aan kimyakimya. Isipokuwa tu kama hakuna yeyote anayemshawishi au walioko pale wakawa wanapenda hivo asome kwa sauti kwa sababu wao wenyewe hawajui kusoma na wanapenda waisikilize kutoka kwa mwengine. Katika hali hizo hakuna neno. Lakini kwa sharti asiwepo yeyote katika walioko msikitini ambaye hajishughulishi na kumsikiliza. Hapo haifai. Haifai kwa mtu kusoma Qur-aan kwa sauti ya juu msikitini na pembezoni mwake yuko ambaye anamshawishi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwatokea Maswahabah zake na wao wanaswali na wanasoma kwa sauti akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kila mmoja wenu anamnong´oneza Mola wake. Hivyo wamoja wasisome Qur-aan kwa sauti juu ya wengine” au alisema “wasisome kisomo.”

Hadiyth hii ni Swahiyh, kama alivosema Ibn ´Abdil-Barr.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (10) http://binothaimeen.net/content/6740
  • Imechapishwa: 22/11/2020