Shiy´ah al-Jazaairiy anamtuhumu Abu Bakr na ´Umar ukafiri

Usishangazwe na kisa hiki, kwa sababu imepokelewa katika mapokezi maalum ya kwamba Abu Bakr alikuwa akiswali nyuma ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na sanamu limetundikwa shingoni mwake na akilisujudia.

Yaziyd bin Mu´aawiyah alimtumia barua ifuatayo Ibn ´Umar:

“Kutoka kwa ´Umar bin al-Khattwaab kwenda kwa Mu´aawiyah bin Sufyaan

Tambua, ee Mu´aawiyah, ya kwamba Muhammad alitujia kwa uongo, uchawi na ametukataza kumwabudu al-Laat, al-´Uzzaa na kuzielekeza nyuso zetu kueleka Ka´bah ambayo alidai kwamba ndio Qiblah cha kiislamu. Huu ulikuwa ndio uchawi wake uliofika kilele ambao kwao alimyakinisha Muusa, ´Iysaa na wana wa israaiyl wengine wote waliobaki. Hata hivyo tuko katika dini ileile tuliyokuwemo hapo kabla, hatujamwacha al-Laat, al-´Uzzaa wala al-Hubal.”

  • Mhusika: Ni´matullaah bin Muhammad al-Jazaairiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Anwaar an-Nu´maaniyyah (1/62)
  • Imechapishwa: 07/12/2018


Takwimu
  • 315
  • 373
  • 1,819,083