Shirki ndogo inamtoa mwenye nayo nje ya dini?

Swali: Je, shirki ndogo inamtoa mwenye nayo nje ya dini?

Jibu: Shirki ndogo haimtoi mtu nje ya dini. Bali inapunguza imani na inapingana na ukamilifu wa Tawhiyd ambayo ni wajibu. Kwa mfano mtu akisoma Qur-aan kwa kujionyesha, akatoa swadaqah kwa ajili ya kujionyesha na mfano wa hayo imani yake inapungua na kudhoofika. Aidha anapata dhambi kwa kitendo hichi. Lakini hakufuru ukafiri mkubwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (08/394)
  • Imechapishwa: 26/06/2021