Shaykh-ul-Islaam kuhusu hukumu ya swalah ya ´iyd

Swali: Shaykh-ul-Islaam anaonelea kuwa swalah mbili za ´iyd ni wajibu…

Jibu: Ndio, anaonelea kuwa ni faradhi kwa watu wote. Shaykh-ul-Islaam amechagua kauli inayosema kuwa swalah ya ´iyd ni faradhi kwa watu wote na sio faradhi kwa baadhi ya watu.

Swali: … ni ipi dalili yake juu ya hilo na kauli yake ina nguvu au haina nguvu?

Jibu: Kauli yake ina nguvu. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha mpaka mwanamke mwenye hedhi kumtoa kwenda kushuhudia swalah ya ´iyd. Ameamrisha watolewe. Hii ni dalili inayoonesha kuwa ni faradhi kwa watu wote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-6-7.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2014