Mimi sipingi kuwepo makundi mengi yaliyo na malengo mbalimbali. Mimi sipingi kuwepo kundi ambalo limejichukulia jukumu la kusahihisha ´Aqiydah za waislamu, uelewa wao na ´ibaadah zao na hawajishughulishi na mazoezi. Kwa hayo nasema kuwa sipingi kuwepo kwa kundi lililojichukulia mazoezi kwa lengo la kuwafanya waislamu kuwa na nguvu kimwili, kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendwa zaidi na Allaah kuliko muumini dhaifu – na kwa wote wawili kuna kheri.”[1]

Sipingi kuwepo kundi lililojichukulia uchumi, lingine lililojichukulia siasi na kadhalika. Hata hivyo ninashurutisha sharti moja; nayo ni kwamba hawa wote washirikiane katika mzungiko wa Uislamu na kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah. Ama kuyaacha makundi kila limoja liwe katika maeneo yake bila ya kuwafungamanisha na Qur-aan na Sunnah ina maana ya kwamba ni kukubali Ummah kufarikiana na kuona mfarakano ulio na muhuri wa Kishari´ah licha ya kuwa uhakika wa mambo jambo hilo linaenda kinyume na Qur-aan na Sunnah.

[1] Muslim (2664).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (34)
  • Imechapishwa: 11/02/2017