Shahaadah kwanza au kutawadha?

Swali: Kafiri aliyesilimu aanze kutamka shahaadah au atawadhe kwanza?

Jibu: Aanze kutamka shahaadah kisha ndio atawadhe kwa ajili ya kuswali. Kuoga juu yake ni jambo lililowekwa katika Shari´ah kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamrisha baadhi ya Maswahabah kufanya hivo waliposilimu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (01/43)
  • Imechapishwa: 06/10/2020