Swali: Katika baadhi ya nchi wanawalazimisha watu kutoa Zakaat-ul-Fitwr pesa. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Dhahiri ni kwamba mtu akilazimishwa kutoa Zakaat-ul-Fitwr pesa basi atoe kuwapa na wala asiwaasi watawala. Lakini hata hivyo atoe kwa uficho yale aliyoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Atoe Swaa´ ya chakula. Kwa sababu serikali kuwaamrisha watu watoe Zakaat-ul-Fitwr pesa ni kuwalazimisha kitu ambacho si Allaah wala Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawakukiweka katika Shari´ah. Na hapo itakulazimu kutoa kile unachoonelea kuwa ndio cha wajibu kwako. Toa chakula na pesa ulizolazimishwa na wala usimuasi mtawala.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/281-282)
  • Imechapishwa: 23/06/2017