Ndugu! Tunaona watu wengi wanapoanza wanajifanya ni watu wa Ikhlaasw. Baada ya hapo kupitia matendo na maneno yake inakudhihirikia yenye kwenda kinyume na Da´wah yake. Tamahaki utamuona ameiuza dini yake. Wema na uongofu aliyokuwemo jana anayauzulu kwa ajili ya dunia. Jana ulikuwa humuoni isipokuwa na watu wa haki na uongofu, Ahl-us-Sunnah wal-Hadiyth. Lakini hii leo unamuona amebadilisha na kugeuza mambo yote. Ghafla wamuona amekuwa kinyume na ile hali yake ya kwanza. Baada ya kuwa na wanachuoni wa Sunnah na Athar, ghafla wamuona amekuwa nyuma ya dunia. Unamuona anatembea na fulani na fulani miongoni mwa watu amabo tunawajua kuwa na u-Hizbiyyah na Bid´ah. Afadhali angelikomeka hapa tu. Bali baada ya hapo anavuka na kutafuta hoja ya matendo yake. Hatimaye wamuona aanza kuwaponda wanachuoni wa Sunnah na Hadiyth, ambao walikuwa ni waalimu zake jana. Haya anayafanya pale ambapo ameshapata yale anayoyataka kwa watu wale alioungana nao. Hivi sasa ameshaipata dunia. Jana alikuwa ni mtu asiyekuwa na maana yoyote, lakini hii leo amekuwa na gari kubwa na nguvu. Amepata dunia kwa kuiuza dini yake; kwa kuacha Sunnah na Ahl-us-Sunnah na kujiunga na Bid´ah na Ahl-ul-Bid´ah.

Halafu utamuona anaanza kujitolea nyudhuru za ki-Ibliys. Ghafla utamsikia akisema ´watu hawa wana msimamo mkali`, ´hawa wana uchupaji wa mipaka`, ´hawa kazi yao ni kuwaponda wengine`, ´hawa wanatofautiana na wengine`. Matokeo yake huyu anakuwa mpinzani mkubwa wa Sunnah na Ahl-us-Sunnah na mzushi wa asli. Sisemi haya kwa kubahatisha, bali ndio uhalisia wa mambo yenyewe. Tumeshuhudia yote haya.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=5503
  • Imechapishwa: 27/08/2020