Salafiyyah ni kundi la Allaah


Swali: Je, Salafiyyah ni kipote (Hizb) na inajuzu…

Jibu: Salafiyyah ndio msingi na sio kipote. Ndio msingi. Ndio msingi na yote yenye kwenda kinyume nayo ni batili. Ni kweli kwamba kinaweza kuitwa Hizb kwa sababu Allaah anasema:

أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ

“Hao ndio kundi la Allaah.” (58:22)

Tunasema kuwa ni kweli kwamba ni kikundi, lakini ni kundi la Allaah. Yenye kwenda kinyume nayo ni kundi la Shaytwaan, kama alivyosema Allaah:

أُولَـٰئِكَ حِزْبُ الشَّيْطَانِ

“Hao ndio kundi la shaytwaan.” (58:19)

Ama kusema tu kuwa Salafiyyah ni kipote halafu ukanyamaza, si sawa. Salafiyyah ni kundi la Allaah kwa sababu Allaah amewaita kuwa ni “kundi la Allaah”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=122012
  • Imechapishwa: 06/09/2020