Swali: Sisi tuna kijana Salafiy ambaye daima hupunguza ndevu zake. Tunamnasihi mara endelevu lakini hata hivyo anapuuza. Je, tumkate kutokana na maasi yake?

Jibu: Hili ni janga na maradhi yaliyoenea. Ni jambo linalosikitisha. Ni jambo linalofanywa na wengi wanaojinasibisha na Sunnah. Baadhi ya ambao wanajinasibisha na Sunnah wananyoa ndevu zao. Ikiwa kufanya hivo kunamfaa, basi hakuna neno akakatwa. Hili ni kuhusu yule anayenyoa ndevu zake au anapunguza. Kwa sababu akipunguza ndevu zake anajifananisha na mayahudi na Raafidhwah:

”Yule anayejifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Ikiwa ananyoa, basi anafanana na mayahudi na manaswara. Na ikiwa anapunguza, basi anafanana na Raafidhwah na mayahudi:

”Yule anayejifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Kwa hivyo ajitakase kujifananisha na makundi haya mawili ambao ni maadui wa Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Kitabu Chake.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=-Ax1nne4_Mc
  • Imechapishwa: 25/12/2020