Swali: Katika chuo kikuu chetu kumefunguliwa kipengele ambapo kunafunzwa ´Aqiydah ya Ashaa´irah. Tunaweza kusoma kwa ajili ya kupata shahada ili tuweze kutimiza masomo yetu katika nchi hii?

Jibu: Ni sawa kusoma fikira za Ashaa´irah na wengineo ili kutambua ubatili wake na kuziraddi. Sisi wenyewe tulizisoma katika selibasi zetu kwa ajili ya kuzitambua na namna ya kuziraddi. Hakuna neno kuyatambua mambo haya.

Huyasomi kwa ajili uyaamini au uyasapoti. Unayasoma ili uyaraddi.

Kunasomwa fikira za Jahmiyyah, Ashaa´ira na Mu´tazilah ili mtu aweze kutambua ubatili wake na namna ya kuyaraddi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (31) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathyl%20majd%20-%2026%20-%2010%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017