Operesheni kwa ajili ya kuondosha kidole kilichozidi

Swali: Mimi nina mtoto amezaliwa akiwa na vidole sita kwenye kitanga chake kimoja. Daktari ameona kuwa kuna muumbuko na hivyo kunahitajika kuondoa kile kidole kilichozidi kwa kufanyiwa operesheni. Ni ipi hukumu ya Shari´ah juu ya kuondosha kidole hichi?

Jibu: Hakuna neno kufanya hivo. Ni sawa kuodoa muumbuko ikiwa hilo halipelekei kumletea mtu madhara na wala hakuna khatari. Bali ndivyo inavyotakiwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (6) http://alfawzan.af.org.sa/node/14379
  • Imechapishwa: 25/11/2016