Swali: Nilinuia endapo Allaah atanitunuku mwana nitampa jina la “Nuuh”. Pindi Allaah aliponiruzuku mwana nikampa jina la “´Abdur-Rahmaan”. Kisha akafariki baada ya kufikisha miaka kumi na mbili. Je, nina dhambi kwa kubadilisha nia?

Jibu: Haina neno. Una khiyari. Unaweza kumpa jina la “Nuuh” au “´Abdur-Rahmaan”. Hakuna neno. Huna dhambi kwa hilo. Nia haikulazimishi kitu. Lakini lau ungeliapa kwa jina la Allaah ya kwamba ungempa jina la “Nuuh”, unatakiwa kutambua kuwa kiapo sio mamoja na nia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340126_0.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020