Nichukue pesa zilizochumwa kwa njia ya haramu?

Swali: Nikijua kuwa kuna mtu ambaye amechuma pesa kwa njia ya haramu na anataka kujikwamua na pesa hizo. Inajuzu kwangu kuchukua pesa hizo kwa ajili ya haja zangu?

Jibu: Ikiwa una haja hakuna neno. Hakuna tofauti kati yako wewe na wengine. Hazichukuliwi kwa kuzingatia kuwa ni swadaqah, zinachukuliwa kama pesa zisizokuwa na mmiliki ambazo zinatumiwa katika mambo ya manufaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (5) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–01041434.mp3
  • Imechapishwa: 07/11/2016