Swali: Ni ipi hukumu ya dini juu ya kile kinachoitwa ´sikukuu ya wapendanao` ambayo hufanywa na watoto wengi wa waislamu katika masiku haya?

Jibu: Hapana shaka kwamba hizi ni miongoni mwa sikukuu zilizozuliwa na zilizoharamishwa. Haijuzu kushirikiana na washirikina wala kuafikiana nao katika sikukuu zao. Chukua fatwa kutoka kwa Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn[1], Shaykh ´Abdullaah bin Jibriyn[2] na wengineo. Vivyo hivyo yale yanayofanywa na baadhi ya wanawake wema katika kutoa mawaidha. Yote hayo ni mazuri. Mambo hayo yanatakiwa kueneza kati ya watu. Ni mamoja kwenye majarida au katika magazeti. Pengine Allaah akanufaisha kupitia mambo hayo.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/imaam-ibn-uthaymiyn-kuhusu-siku-ya-wapendanao/

[2] Tazama https://firqatunnajia.com/category/makala/manhaj/5-msimamo-kwa-wapinzani-na-madhehebu-yao/an-najmiy-msimamo-kwa-ahl-ul-bidah/ahmad-an-najmiy-akimjibu-ibn-jibriyn/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 01/11/2020