Ibn ´Uthaymiyn kuhusu siku ya wapendanao

Swali: Hivi karibuni sherehe ya Siku ya wapendanao imeenea na khaswa baina ya wanafunzi wa kike. Ni sikukuu ya kinaswara. Watu wanavaa nguo nyekundu na wanapeana mauwa mekundu (roses). Tunataraji kwamba unaweza kutubanishia hukumu ya sikukuu hii na kuwapa Waislamu nasaha.
Jibu: Haijuzu kusherehekea siku ya wapendanao kutokana na sababu zifuatazo:
1- Ni sikukuu iliyozushwa ambayo haina msingi wowote katika Shari´ah.

2- Inapelekea katika mapenzi na tamaa.

3- Inapelekea moyo kushughulishwa na suala hili ambalo linakwenda kinyume na uongofu wa Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum).

Kwa hivyo haijuzu kuzusha sherehe yoyote siku hii, sawa ikiwa inahusiana na chakula, kinywaji, nguo, zawadi au mfano wa hayo.

Muislamu anatakiwa kuwa na nguvu katika Dini yake na asiwe ni mwenye kufuata kila kitu na watu wote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (16/199)
  • Imechapishwa: 14/02/2017