Swali: Ni ipi hukumu ya ibara hii “Qur-aan imesema kadhaa”?

Jibu: Uhakika wa mambo ni kwamba Qur-aan haisemi, bali ni Maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Mwenye kuzungumza ni Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Badala yake inatakiwa kusema “kumesemwa kadhaa katika Qur-aan, Allaah Amesema kadhaa” na bora zaidi ni kusema “Allaah Amesema kadhaa”. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema katika Hadiyth Qudsiy “Allaah Amesema kadhaa”. Kadhalika Salaf walipokuwa wanatumia dalili kwa Aayah wanasema “Allaah Amesema na Mtume wa Allaah amesema”.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26882
  • Imechapishwa: 19/05/2015