Ni picha zipi zinazowazuia malaika kuingia nyumbani?

Swali: Picha iliyoko kwenye simu inaingia ndani ya maneno yake Mtume (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam):

“Malaika hawaingii katika nyumba ilio na mbwa au picha”?

Jibu: Hadiyth inalenga picha iliowekwa wazi au iliyotundikwa. Kuhusu picha ambayo imefichikana na haionekani haiingii ndani ya hukumu hii.

Lakini hata hivyo haijuzu kutumia simu ilio na camera. Ni kifaa cha picha. Haifai kununua kifaa cha picha na kukihifadhi. Badala yake ni wajibu kukivunja. Kwa kuwa ni kifaa cha shari.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (11) http://alfawzan.af.org.sa/node/2054
  • Imechapishwa: 15/02/2017