Ni lini mtu anahesabika kuwahi Rak´ah kwenye Rukuu´?

Swali: Nikiingia na imamu amerukuu, kisha nikasema “Allaahu Akbar”. Wakati nilipokuwa ninaenda katika Rukuu´ imamu akainuka. Je, nahesabika nimewahi Rak´ah?

Jibu: Mikono yako ikiwahi kwenye magoti kabla ya imamu kuinuka, umewahi Rukuu´. Ama akiinuka kabla ya mikono yako kufika kwenye magoti, Rukuu´ imekupita.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14221
  • Imechapishwa: 17/11/2014