Ni kweli anayesoma du´aa hii ataruzukiwa mtoto?


Swali: Kuna mtu mmoja amejitokeza katika chaneli na kusema “Atayesema kwenye Sujuud:

رَبِّ لَا تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ

“Mola wangu! Usiniache pekee; Nawe ndiye Mbora wa wenye kurithi.” (21:89)

mara arubaini, basi ataruzukiwa mtoto. Anasema kuwa hili ni jambo ambalo limejulikana kwa uzowefu. Ni ipi dhwaabit katika hilo na kauli hii ni sahihi?

Jibu: Huu ni uzowefu wake yeye. Huu ni uzowefu wake yeye ikiwa kama ni mkweli na sio Shari´ah iliyowekwa. Hakuwekwi katika Shari´ah kwa mambo kama haya. Hii ni Bid´ah. Hii ni Bid´ah:

“Kila Bid´ah ni upotevu.”

Kadhalika hakusomwi Qur-aan katika Sujuud.

رَبِّ لَا تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ

“Mola wangu! Usiniache pekee; Nawe ndiye Mbora wa wenye kurithi.” (21:89)

Hii ni Aayah katika Qur-aan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1430-10-15.mp3ti
  • Imechapishwa: 15/11/2014