Ni jitu gani linawatukana Maswahabah wa Mtume wa Allaah?


Swali: Ni ipi hukumu kwa wale wenye kuvuka mipaka kwa baadhi ya Maswahabah na wanatukana wengine na wakati mwingine wanaweza kuwakufurisha baadhi ya Maswahabah na kumtuhumu uzinzi mama wa waumini ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa)?

Jibu: Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) ndio viigizo, watu bora kabisa na wahange wa Ummah. Mwenye kuwatukana anautukana Uislamu. Kwa sababu wao ndio ambao wametunukulia Uislamu kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wao ndio walio kati na kati baina yetu sisi na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wao ndio ambao wamemnusuru Mtume na wakapigana Jihaad wakiwa naye bega kwa bega na wakajitolea roho na mali zao. Wao ndio ambao waliunusuru Uislamu baada ya kufa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mashariki na maghariib. Wao ndio ambao walifunza utu na elimu yenye manufaa ambayo waliirithi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni jitu gani hili linawatukana? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwatukane Maswahabah zangu! Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, lau mmoja wenu atatoa dhahabu kiasi cha mlima wa Uhud basi hatofikia robo wala nusu ya mmoja wao.”

Lau wewe utatoa swadaqah dhahabu kiasi na mlima wa dhahabu haitofikia sawa na thawabu za Swahabah mmoja akitoa swadaqah kiasi na robo ya chakula au nusu yake. Hili ni kutokana na fadhila zao na hadhi yao.

Yule asiyemtakasa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwa yale Allaah aliyomtakasa nayo ni mwenye kumkadhibisha Allaah, Mtume Wake na maafikio ya waislamu. Hivyo huyu ni kafiri na tunaomba Allaah atukinge.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13379
  • Imechapishwa: 29/04/2018