Ni jambo baya zaidi kuchukua picha Haram

Swali: Ni ipi hukumu ya kuchukua picha kwa camera na kwa simu Haram?

Jibu: Kuchukua picha viumbe vyenye roho, kukiwemo wanadamu, ni haramu mbaya zaidi na dhambi kubwa. Ni mamoja hilo limefanywa kwa camera, kwa simu au zana nyingine. Dalili ya hilo ni kuenea kwa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kila mtengeneza picha atakuwa Motoni. Ataifanya kila picha aliyoitengeneza kuwa na nafsi ambapo ataadhibiwa kwayo Motoni.”[1]

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) amesema: “Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule ambaye anajaribu kuumba mfano wa viumbe Wangu? Hebu waumbe mdudu chungu, waumbe punje ya nafaka au waumbe chembe ya shayiri.”[2]

Bi maana watengeneza picha. Wanajaribu kuleta picha inayofanana na kiumbe alichoumba Allaah. Hadiyth inajulisha kuwa mfanyaji picha ndiye dhalimu mkubwa zaidi, kwa sababu amemfanyia utovu wa adabu Allaah na amejaribu kwa picha zake kujifananisha na Allaah kuumba na kutengeneza kwake sura. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayetengeneza picha duniani atakalifishwa kuipulizia roho siku ya Qiyaamah, jambo ambalo hatoweza.”[3]

Kwa hiyo ni lazima kwa muislamu kumcha Allaah na aache jambo la picha kwa sampuli zake zote; kwa kutumia zana ya picha, kuchora, kuchonga na kadhalika. Kwa sababu Hadiyth zimekuja kwa jumla zinawazokemea kwa ukali wafanyaji picha. Hata hivyo kuchukua picha Haram ni jambo baya zaidi kwa sababu ni kudhihirisha dhambi katika msikiti Mtakatifu. Kwa mujibu wa Hadiyth hizi na nyenginezo nyingi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) picha ni katika dhambi kubwa.

[1] Muslim (2110).

[2] al-Bukhaariy (5953) na (7559) na Muslim (2111).

[3] al-Bukhaariy (5963) na Muslim (2110).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=VPTBYa9MNFM
  • Imechapishwa: 07/07/2022