Ni ipi hukumu ya mwenye kusoma Tashahhud ya mwisho katika Tashahhud ya kwanza?

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusoma Tashahhud ya mwisho katika Tashahhud ya kwanza?

Jibu: Katika ile ya kwanza afupike katika Tashahhud na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusu kuomba ulinzi dhidi ya Moto ni jambo linalokuwa katika Tashahhud ya mwisho. Akiikamilisha katika ile Tashahhud ya kwanza hakuna juu yake kitu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 25
  • Imechapishwa: 24/07/2018