Ibn Baaz kuhusu Tasliym mbili zote ni nguzo katika swalah

Swali: Ni yepi maoni yako kwa yule ambaye ametofautisha kati ya Tasliym mbili na akasema kwamba Tasliym ya kwanza ndio nguzo na Tasliym ya pili ni sunnah?

Jibu: Ni wajibu kuileta. Wanachuoni wengi wanaona kuwa nguzo ni ile Tasliym ya kwanza. Lakini maoni yenye nguvu ni yale yaliyosema mwandishi kwamba Tasliym zote mbili. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitoa Tasliym mbili. Isitoshe amesema:

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 25
  • Imechapishwa: 24/07/2018