Ni ipi hukumu ya kuchora kiumbe chenye roho kwa mkono?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuchora kwa mkono?

Jibu: Kuchora kwa mkono ni haramu. Bali ni katika madhambi makubwa. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengenezaji picha. Kulaaniwa hakukuwi isipokuwa juu ya dhambi kubwa. Ni mamoja picha hiyo imechorwa kwa ajili ya majaribio ya ubunifu fulani, kwa ajili ya kuwaonyesha wanafunzi au mengineyo. Ni haramu. Lakini hata hivyo hakuna neno endapo kutachorwa kiungo peke yake cha mwili kama vile kuchora mkono peke yake au kichwa peke yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/285)
  • Imechapishwa: 01/06/2017