Swali: Ni ipi hukumu ya kuhifadhi picha kwa sababu ya kumbukumbu?

Jibu: Kuhifadhi picha ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekhabarisha ya kwamba Malaika hawaingii ndani ya nyumba iliyo na picha. Hii ni dalili inayofahamisha juu ya uharamu wa kuhifadhi picha ndani ya majumba.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/283)
  • Imechapishwa: 31/05/2017