Ndio maana wanamchukia Jibriyl


Swali: Mayahudi wanamchukia Jibriyl (´alayhis-Salaam) kwa sababu wanaona kuwa yeye ndiye analeta vita?

Jibu: Wao wanadai hivi. Jibriyl (´alayhis-Salaam) huleta kheri. Huleta Wahy. Yeye ndiye amepewa kazi ya kuteremsha Wahy ambao uko na kheri na uhai.

Katika Shiy´ah wako wanaosema kuwa ´Aliy ndiye alitakiwa kupewa utume lakini hata hivyo Jibriyl akafanya khiyana na badala yake akaenda nao kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa ajili hii ndio maana wanamchukia Jibriyl (´alayhis-Salaam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (70) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighatsah%20-%2019%20-0%207%20-%201438.mp3