Nasaha kwa wazazi wasiotaka kuwaoza mabanati wao

Niliwahi kuelezwa hapo kitambo ya kwamba kuna mtu ambaye alikuwa hawatoi wasichana wake wakubwa kuwaoza. Mmoja wao akaumwa. Pengine vilevile aliugua kwa sababu ya kuzuiwa kuolewa – Allaah ndiye mjuzi zaidi ya hili. Kabla ya kukata roho na mbele yake kulikuwa wanawake wengine, akawapa ujumbe:

“Mwambieni baba yangu miadi yangu mimi na yeye ni siku ya Qiyaamah nitaposimama nae mbele ya Allaah.”

Namna hii ndio alimwambia baba yake. Hata kama asingemwambia hivi huu ndio uhakika wa mambo. Hata kama asingemwambia hivi mwanamke huyu atakuwa mgomvi wake siku ya Qiyaamah ambayo kila mmoja atamkimbia mwenzie.

Nasaha zangu kwa walezi wa wanawake: wamche Allaah (´Azza wa Jall) na wasiwazuie wanawake kwa wale ambao ni haki kwao kuwaoza kwa ambaye kumeridhiwa juu yake dini na tabia yake. Ana haki ya kumkatalia ikiwa atamchagua ambaye hana dini na tabia. Lakini amemchagua mwanaume ambaye ana dini njema na tania nzuri kisha akamkatalia pasi na sababu, ni kitendo cha haramu, dhambi na khiyana. Sababu yoyote itayopelekea akaharibika madhambi anapata yeye – yaani huyu mlezi wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (07)
  • Imechapishwa: 01/05/2020