Namna ya kurudisha mazuri zaidi katika salamu

Swali: Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا

“Mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo.” (04:86)

Ikiwa mtu atanisalimia kwa kusema:

“as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh”

ni vipi nitazidisha?

Jibu: Unazidisha kwa kumwambia:

“Allaah akujaze kheri.”

“Allaah akusamehe.”

“Allaah akubariki.”

“Allaah akufanyie vizuri.”

unamwombea du´aa na mfano wa hivo. Kuzidisha huku ni vizuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21554/كيف-تكون-زيادة-الرد-على-السلام-الكامل
  • Imechapishwa: 20/08/2022