Swali: Mtu akimuona mmoja katika ndugu zake anatenda dhambi ashike msimamo gani?

Jibu: Ni wajibu kwake kukataza maovu kwa njia nzuri, maneno mazuri, ya upole na ya ulaini kwa yule anayefanya maovu hayo. Pengine akawa ni mjinga. Anaweza kuwa ni mtu mwenye maadili magumu na wakati utamkemea kwa ukali basi maovu yake yakazidi. Ni wajibu kwake kukemea maovu kwa njia na maneno mazuri. Dalili za wazi ni kumnukulia yale yaliyosemwa na Allaah na Mtume wake pamoja na kumuombea du´aa ya mafanikio ili asiweze kukimbia. Hivi ndivyo anavyokuwa mwenye kuamrisha mema na mwenye kukataza maovu. Anatakiwa vilevile kuwa na elimu, umaizi, upole na uvumilivu ambayo yatamfanya yule anayemkemea akubali kutoka kwake na wala asifanye ukaidi. Yule mwenye kuamrisha mema na kukataza maovu anatakiwa kujitahidi kutumia matamshi ambayo kwayo kunatarajiwa kukubaliwa haki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/233)
  • Imechapishwa: 03/07/2017