Namna ambavo inatakiwa kuanza Khutbah ya ´iyd


Swali: Je, imepokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifungua Khutbah yake ya ´iyd kwa kusema:

الله أكبر الله أكبر الله أكبر

“Allaah ni mkubwa, Allaah ni mkubwa, Allaah ni mkubwa.”?

Jibu: Hapana.

Swali: Kwa hivyo yale yanayofanywa na wahubiri wengi ni…

Jibu: … hayana msingi. Hata hivyo tunaweza kusema kuwa yamepokelewa kama ambavo pia tunaweza kusema kuwa hayakuthibiti. Kwa msemo mwingine ni kwamba yamepokelewa, lakini hata hivyo hayakusihi kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akileta Takbiyr kipindi cha Khutbah. Haya yanapatikana katika “as-Sunan” ya Ibn Maajah, lakini cheni ya wapokezi wake ni dhaifu na si Swahiyh. Kuhusu ufunguzi, itambulike kuwa hakuna tofauti kati ya Khutbah ya ´iyd na Khutbah ya ijumaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (548)
  • Imechapishwa: 18/09/2020