Leo kuna mwenye kuwakumbatia Ahl-ul-Bid´ah hawa, anawapenda, anawatetea, anatetea Bid´ah zao, wanawatukana Maswahabah, wanawatukana Mitume, wanasema Wahdat-ul-Wujuud, ujamaa [socialism] na kadhalika. Wana majanga mengi kabisa. Pamoja na hivyo watu hawa wamesimama upande wao na wanawaita kuwa ni “Mujaddidiyn”. Wana Bid´ah zenye kujaa makapu ukilinganisha na Bid´ah za Khawaarij. Sisi tuko wapi na kundi hili lililookoka, Firqat-un-Naajiyah?

Ninawaulizeni kwa Jina la Allaah: yule aliyesimama upande wa Raafidhwah ambao wanawatukana Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Suufiyyah kwa upotevu wao mbali mbali na kuwatetea na wakati huo huo anawapiga vita Ahl-us-Sunnah. Je, huyu si katika wao? Amesimama upande wa Ahl-ul-Bid´ah na vitabu vyao ambavyo vimejaa upotevu wa kikafiri. Pamoja na hivyo amesimama upande wao na kuwatetea. Ukiongezea juu ya hilo anapambana kweli kweli na yule mwenye kuwazungumzia watu hawa wa Bid´ah na juu ya vitabu hivyo ilihali anafanya hivyo kwa ajili ya kutoa nasaha kwa ajili ya Allaah. Ni kundi ambalo linatoa nasaha kwa ajili ya Allaah, linatahadharisha shari hii na kutahadharisha Bid´ah hii kwa kumuiga Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Salaf-us-Swaalih. Kisha kunakuja watu hawa na kuwatupia tuhuma na kuwapiga vita na wakati huo huo wanasema na wao kuwa ni Ahl-us-Sunnah, wenye kumnusuru Allaah, wanasema kuwa Sayyid Qutwub ni Mujaddid, [Hasan] al-Bannaa ni Mujaddid na al-Mawduudiy ni Mujaddid ilihali watu hawa ni Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba Khawaarij hawakufikia Bid´ah na upotevu waliofikia watu hawa. Hivi hapa vitabu vyao tunapawa changamoto. Wale Khawaarij ambao ´Aliy aliwapiga vita, hata Khawaarij wanaopatikana hii leo hawana Bid´ah kama za Sayyid Qutwub. Lau utahesabu Bid´ah za Khawaarij wa leo hutopata kitu ukilinganisha na Bid´ah zinazopatikana kwa Sayyid Qutwub. Sayyid Qutwub amekusanya Bid´ah kwa sampuli zake zote katika vitabu vyake. Sayyid Qutwub anajionyesha kuwa ana hamasa juu ya Uislamu ilihali anaufanyia Takfiyr Ummah kuanzia Maswahabah mpaka hii leo. Khawaarij hawakufanya haya. Pamoja na yote haya bado tunasema kuwa ni “Mujaddid” na “Imaam” na ukiongezea juu ya hayo tunamtetea na kutetea vitabu vyake. Je, watu hawa kweli wanahesabika katika Sunnah na ni Twaafat-un-Mansuurah? Hapana. Ni juu yao kutubu kwa Allaah na wafuate mfumo wa Salaf juu ya kushika msimamo sahihi dhidi ya Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kutoka kitabu “Firqat-un-Naaniyah – misingi na I´tiqaad zake
  • Imechapishwa: 14/07/2020