Mwenye istihaadhah anataka kuoga kunapoingia kila swalah


Swali: Mwenye damu ya ugonjwa akiweza kutawadha katika kila swalah, inajuzu kwake kujumuisha swalah katika hali hii?

Jibu: Nadhani anachokusudia ni kuoga [katika kila swalah]. Kutawadha? Kutawadha ni wajibu kwa kila swalah. Lakini kuhusu kuoga, hili ndilo linatakiwa kuangaliwa. Akiweza kuoga kila kunapoingia kila swalah, ni sawa hakuna neno.