Mwanamke mfungaji anaona maji ya uchafu-uchafu

Swali: Kuna mwanamke alijiwa na hedhi na damu ikakoma katika siku ya sita. Hakuna damu iliyoonekana tangu juwa lizame mpaka 24:00. Matokeo yake akajitwaharisha na kufunga siku ya kufuata. Siku hiyo hiyo akapata maji ya uchafu-uchafu. Je, damu hiyo inahesabika kuwa ni hedhi pamoja na kuzingatia ya kwamba damu yake humjia kwa siku saba?

Jibu: Maji ya uchafu-uchafu sio katika hedhi. Maji ya uchafu-uchafu inayomjia mwanamke baada ya kusafika hauzingatiwi kitu. ´Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Tulikuwa hatuzingatii maji ya uchafu-uchafu kuwa ni kitu baada ya kusafika.”[1]

Katika upokezi mwingine:

“Tulikuwa hatuzingatii maji ya uchafu-uchafu baada ya kutwaharika kuwa ni kitu.”[2]

Hedhi sio maji ya uchafu-uchafu wala maji ya umanjano. Kujengea juu ya hili swawm ya mwanamke huyo ni sahihi, sawa siku ile ambayo hakuona maji ya uchafu-uchafu na siku aliyoona maji ya uchafu-uchafu. Kwa kuwa maji ya uchafu-uchafu sio hedhi.

[1] Abu Daawuud (307).

[2] al-Bukhaariy (326).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/105)
  • Imechapishwa: 03/06/2017