Mwanamke mfungaji amepata ada yake wakati wa adhuhuri


Swali: Hedhi ya mwanamke imekuja kipindi cha adhuhuri. Je, ni lazima kwake kufungua au akamilishe funga yake mpaka wakati wa magharibi?

Jibu: Anatakiwa kufungua pale tu atakapopata hedhi hata kama ni muda kidogo tu kabla ya jua kuzama. Hata hivo atalazimika kuilipa siku hiyo. Lakini akipata ada yake baada ya jua kuzama, swawm yake ni sahihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin Humayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Ibn Humayd, uk. 174
  • Imechapishwa: 05/05/2021