Mwanamke kusema katika du´aa ”mja wako”


Swali: Katika baadhi ya Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imekuja:

”Hakuna mja atakayefikwa na hamu au huzuni kisha akasema:

اللّهُـمَّ إِنِّي عَبْـدُكَ، ابْنُ عَبْـدِكَ، ابْنُ أَمَتِـكَ نَاصِيَتِي بِيَـدِكَ، مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤكَ، أَسْأَلُـكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ، سَمَّـيْتَ بِهِ نَفْسَكَ، أِوْ أَنْزَلْتَـهُ فِي كِتَابِكَ، أَوْ عَلَّمْـتَهُ أَحَداً مِنْ خَلْقِـكَ، أَوِ اسْتَـأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الغَيْـبِ عِنْـدَكَ، أَنْ تَجْـعَلَ القُرْآنَ رَبِيـعَ قَلْبِـي، وَنورَ صَـدْرِي، وجَلَاءَ حُـزْنِي، وذَهَابَ هَمِّـي

”Ee Allaah! Hakika mimi ni mja Wako, mwana wa mja Wako, mwana wa mjakazi Wako, utosi wangu uko mikononi Mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako, ni adilifu kwangu unihukumu kwayo, nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako; ulilojiita kwalo Mwenyewe, uliloliteremsha katika Kitabu Chako, ulilomgunza nalo yoyote katika viumbe Vyako, ulilolificha katika elimu ya ghaibu Kwako: nakuomba uifanye Qur-aan kuwa ni uhuisho wa moyo wangu, nuru ya kifua changu na ufumbuzi wa  huzuni yangu.”[1]

Je, mwanamke aseme ”mja wako” (عبدك) au aseme ”mjakazi wako” (أمتك)? Vilevile katika Hadiyth nyenginezo zinazofanana na hii.

Jibu: Jambo ni lenye wasaa Allaah akitaka. Bora ni yeye kusema:

اللّهُـمَّ إِنِّي عَبْـدُكَ، ابْنُ عَبْـدِكَ، ابْنُ أَمَتِـكَ

”Ee Allaah! Hakika mimi ni mjakazi Wako, msichana wa mja Wako, msichana wa mjakazi Wako… ”

Hivi inakuwa ndio sahihi zaidi kwake. Akiomba kwa tamko lililokuja katika Hadiyth basi haitodhuru Allaah akitaka. Kwa sababu, ingawa ni mjakazi (أمة ), yeye pia ni mja miongoni mwa waja wa Allaah.

[1] Ahmad (01/391). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/403)
  • Imechapishwa: 14/02/2021