Mwanamke kusafiri ndani ya eda yake

Swali: Kuna mwanamke ambaye amefiliwa na mumewe na anaishi ar-Riyaadh na hana yeyote. Kaka yake anaishi Makkah. Je, inajuzu kwake kusafiri kwenda kwake na kufanya ´Umrah pamoja na Mahram wake?

Jibu: Hakuna neno ikiwa yuko khatarini, hawezi kubaki mwenyewe na hana yeyote ambaye anaweza kumliwaza. Lakini ikiwa yuko na wa kumliwaza, hayuko katika khatari, yuko na muhudumu wa kike, jamaa zake kama vile mamake mume na wengine wenye kumliwaza na kumwondoshea mawazo, haifai kwake kutoka mpaka pale itakapomalizika eda yake. Ama akiwa analazimika kufanya hivo hapana neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/6369/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B3%D9%81%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D8%AB%D9%86%D8%A7%D8%A1-%D9%81%D8%AA%D8%B1%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%AF%D8%A7%D8%AF
  • Imechapishwa: 27/12/2020