Mwanamke anatwahirika kutwa nzima katika muda wake wa hedhi

Swali: Damu ya mwezi ya mwanamke kawaida huwa kwa muda wa siku saba mpaka nane. Wakati mwingine damu yake inaweza kusita kwa muda wa kutwa nzima haoni damu, kisha inarudi. Afanye kitu gani pindi inapokatika wakati wa ada yake ya mwezi?

Jibu: Kama hakuna kitu kinachokuja kabisa kutwa nzima, anatakiwa kuoga na kuswali siku hii. Muda wa kutwaharika unazingatiwa wakati wa hedhi yake. Ataoga na kuswali. Wakati hedhi yake inaporudi, aache kuswali mpaka atapokamilisha muda wake wa hedhi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14340421.mp3
  • Imechapishwa: 24/09/2020