Swali: Je, madhambi makubwa ni khatari zaidi kuliko Bid´ah ndogo?

Jibu: Hapana. Bid´ah ni khatari zaidi kuliko madhambi kwa kuwa ni kusema juu ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bila ya elimu:

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

“Sema: “Hakika Mola wangu Ameharamisha machafu [yote] yaliyodhihirika na yaliyofichika na dhambi [za kila aina], ukandamizaji bila ya haki na kumshirikisha Allaah kwa [chochote kile] ambayo hakukiteremshia mamlaka na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.”(07:33)

Wanachuoni wanasema kuna matarajio kwa mtenda madhambi akatubu kwa sababu anafanya madhambi kwa sababu ya matamanio na hawaa zimemshinda ambapo hutubia. Hata hivyo mtu wa Bid´ah hatubii. Anaonelea kuwa yuko katika haki. Mtenda madhambi anajua kuwa anafanya madhambi na yuko khatarini. Mtu wa Bid´ah anaona kuwa yuko katika haki; hakubali lolote na hajirudi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf–16041434.mp3
  • Imechapishwa: 24/09/2020