Swali: Huyu dada anasema mume wake anamkata [anamhama] bila ya sababu na kwa masiku mengi analala nje ya nyumba kwa familia yake na humpiga mpaka kavunja mkono na pua lake. Na wala hamhudumii yeye na watoto, na anamsemea uongo kwa familia yake. Nataraji kutoka kwa Shaykh amnasihi na ainasihi familia yake. Pamoja na kuwa [mke huyu] ni mwenye msimamo.

Jibu: Kwa kweli huyu mume, kitendo chake hichi ni makosa. Ima akawa ana kasoro katika akili yake, asiyejua akifanyacho, aliyesibiwa na maradhi kwenye akili yake hafikirii, mtu kama huyu kanyanyuliwa kalamu [haandiiki dhambi]. Ama ikiwa ni katika watu wenye akili na anafikiria, basi hichi ni kitendo cha kimakosa na kiovu. Kuiacha nyumba na kumuacha mke peke yake, ni kitendo kisichoonesha akili za mtu wala Dini yake wala wanaume wake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ

“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya [matumizi] wanayotoa katika mali zao.” (04:34)

Usimamizi wake uko wapi kwa mwenye kuihama nyumba yake kwa masiku mengi na akaacha ahli zake? Usimamizi wake utakuwa wapi kwa mtu ambaye anamhama mke wake kitandani pamoja na kuwa la jibu juu yake ni kumaliza shahawa zake kwa Alichomhalilishia Allaah.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Na kwenye tupu ya mmoja wenu kuna swadaqah.” Wakasema: “Ewe Mtume wa Allaah! Mmoja wetu atayaendea matamanio yake na akawa na ujira kwa hilo? Akasema: “Je, mnaonaje lau angeiweka [tupu yake] kwenye haramu angelipata madhambi? Hivyo akiiweka kwenye halali atakuwa na ujira.”

Mtu kuihama nyumba yake, akawa pamoja na jamaa na marafiki zake katika usiku mkubwa, haya yote ni makosa. Ni bora kwa mtu kubakia kwenye nyumba yake usiku na mke wake na kuichunga nyumba yake, hili ndio la wajibu kwake. Kazi umekalia kufuata kichwa mchunga, wakikaa nawe unakaa, wakisimama nawe unasimama na wala hujui kwa nini, [ukiulizwa kwa nini umefanya? Wasema] ni kwa kuwa watu nao wamefanya.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal ash-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=tblGC_PS1oU
  • Imechapishwa: 22/09/2020