Mtu kumbusu Mahram wake wakati wa mamkuzi

Swali: Je, inafaa kumbusu dada yangu au yeye akanibusu?

Jibu: Hakuna neno ukambusu dada yako au yeye akakubusu. Vivyo hivyo wale Mahaarim zako wote kama vile shangazi yako, mama yako mdogo, mke wa baba yako, mama yako na wapwa wako. Wabusu kwa shavu, pua, paji la uso au kichwa akiwa ni mtumzima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimbusu Faatwimah pindi anapoingia kwake au pindi yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapoingia kwake akiushika mkono wake. Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) alipongia nyumbani kwa msichana wake ´Aaishah ilihali ni mgonjwa alimbusu kwenye shavu lake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (07/187)
  • Imechapishwa: 12/06/2021