Mtu ambaye yuko na madeni analazimika kutoa zakaah?

Swali: Mtu ambaye yuko na madeni analazimika kutoa zakaah au zakaah inaanguka kwake?

Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba akiwa na pesa na ikapitikiwa na mwaka basi wajibu kwake kutoa zakaah hata kama atakuwa na madeni. Kwa mfano mtu ana  10.000 na akataka kulipa deni lake lakini akawa hakufanya hivo mpaka pesa hizo zikafikiwa na mwaka basi anatakiwa kuzitolea zakaah. Mfano mwingine ni kama atakuwa na pesa hizo kwa ajili ya kutaka kuoa, kununua gari, nyumba au chakula kwa ajili ya familia yake na pesa hizo zikapitikiwa na mwaka basi ni wajibu kwake kuzitolea zakaah.

Ama akilipa madeni yake, akaoa au akanunua nyumba kabla ya pesa hiyo kufikisha mwaka basi hakuna kinachomlazimu. Lakini zikipitikiwa na mwaka basi anatakiwa kuzitolea zakaah.

Wapo wanachuoni wengine wenye kuonelea kuwa uwajibu unamwangukia kutokana na yale madeni alonayo. Lakini maoni ya sawa ni kwamba anatakiwa kuzitolea zakaah. Kwa sababu nyoyo za mafukara zimefungana kwa pesa hizo na sababu nyingine tena zimefikiwa na mwaka.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 25/10/2018