Swali: Baba yangu amekufa na ameacha nyumbani kwetu TV. Nimejaribu kuitoa nyumbani lakini mama yangu ameng´ang´ania kuibakiza. Ni zipi nasaha zako kwa mamangu na yeye hivi sasa anakusikiza na wala hakimfichiki kinachoendelea hapa.

Jibu: Nasaha zangu kwake amhimidi Allaah juu ya usalama na amshukuru Allaah kumjaalia mtoto huyu ambaye natarajia kwamba atakuwa mwema. Namnasihi vilevile kuondoa TV nyumbani kwake. Lakini sisemi kuwa ni haramu ikiwa mtu ameingiza TV nyumbani kwake na hatazami isipokuwa taarifa ya khabari, mawaidha na mfano wa hayo. Katika hali hii itakuwa sio haramu. Si haki kwetu kuharamisha ambacho hakuharamisha Allaah (´Azza wa Jall).

Kwa ajili hiyo namnasihi kuondoa TV hii kwa kujengea juu ya maombi ya mtoto wake ambaye nataraji kwa Allaah akawa mwema. Ni sawa badala yake akamnunulia deki na kanda ambapo akawa anamwekea mambo ya manufaa katika mihadhara ya kidini, mazingira na mfano wa hayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1206
  • Imechapishwa: 22/08/2019