Mtazamo wa al-Hajuuriy juu ya Khaliyfah mwongofu ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) kuhusu adhaana ya ijumaa

Miongoni mwa majanga ya mtu huyu ambayo yanaenda kinyume na mfumo wa Ahl-us-Sunnah ni maneno ya kwamba ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) ameleta Bid´ah potevu pindi alipoadhini adhaana ya pili siku ya ijumaa. al-Hajuuriy amesema katika kitabu chake “al-Jumu´ah” chapa ya Daar Imaam Ahmad 249-250:

“Tunamwambia yule aliye na elimu chache kuhusu Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanaoonelea adhaana ya kwanza siku ya ijumaa: Je, adhaana hii ni katika uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye ndiye aliye na uongofu bora kabisa, kama ilivyokuja katika “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia Hadiyth ya Jaabir au ni kitu kilichozuliwa na ´Uthmaan bin ´Affaan, kama ilivyo katika Hadiyth ya as-Saa´ib katika “as-Swahiyh” katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na kama tulivyonukuu maafikiano (Ijmaa´) katika yale tuliyotanguliza kutoka kwa wanachuoni ya kwamba ni kitu kilichozuliwa? Kukisemwa ya kuwa ni katika uongofu wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi huyo ni mwongo mkubwa na hatopata katika wanachuoni wa waislamu anayeafiki uongo huu wenye kutia aibu. Endapo atasema kama wanavyosema wanachuoni wote ya kwamba sio katika matendo ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba ni jambo lililozuliwa kama walivyoafikiana juu ya hilo wanachuoni wa waislamu basi tutamwambia yafuatayo: huoni katika Hadiyth ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakutahadharisha kutokamana na mambo ya kuzuliwa na kusema kuwa ni upotevu?”

Tazama namna anavyoyapeleka maneno yake hatua kwa hatua na namna anavyokariri masuala haya mpaka awafikishe wasomaji kuona kuwa ´Uthmaan ameleta adhaana iliyozuliwa na kila kilichozuliwa ni upotevu. Ee Allaah! Hakika sisi tunajitenga mbali uthibitishaji na msingi huu unaoenda kinyume na maafikiano ya Ummah.

Ninaapa kwa Allaah ya kwamba huku ni kumshambulia ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh). Yeye alikuwa Khaliyfah mwongofu aliyeongozwa kutokana na dalili ya Hadiyth ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni vipi utampachika Bid´ah na kwamba amezua katika dini? Shaykh-ul-Islaam [Ibn Taymiyyah] amesema katika “al-Minhaaj” (06/293):

“Halafu katika maajabu ni kwamba Raafidhwah wanamkemea ´Uthmaan kitu kilichoshuhudiwa na Answaar na Muhaajiruun na hawakumkemea. Bali waislamu wote wakamfuata juu ya adhaana ya ijumaa.”

  • Mhusika: Shaykh ´Arafaat bin Hasan bin Ja´far al-Muhammadiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan al-Fawriy (01/34)
  • Imechapishwa: 03/11/2016