Mtandio wakati wa kusoma Qur-aan?


Swali: Ni lazima kwa mwanamke kujifunika kwa mtandio kichwani wakati wa kusoma Qur-aan na pia wakati wa kutaka kusuhudu sijda ya kisomo?

Jibu: Sijda ya kisomo ni swalah. Anapaswa awe mwenye kujisitiri kama anavokuwa ndani ya swalah. Ama wakati wa kusoma Qur-aan hana ulazima wa kufanya hivo. Isipokuwa ikiwa kama mbele yake wako ambao si Mahram zake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (103) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-6-3-1441_1.mp3
  • Imechapishwa: 20/01/2021